Psalms 10:7-10


7 aKinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.

8 bHuvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.

9 cHuvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.

10 dMateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.
Copyright information for SwhKC